
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeambiwa na Naibu
Kamishna wa Polisi, Kamanda Simon Siro (54), ambaye amedai mahakamani
kwamba alitoa zuio la kuandamana kwenda Ikulu kwa Wanawake wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Bawacha) kwa sababu maandamano hayo
yangesababisha uvunjifu wa amani.
Alitoa
madai hayo, wakati akitoa ushahidi dhidi ya Mbunge Halima Mdee na
wenzake, kwamba baada ya kupitia vigezo vya kiusalama, njia waliyotaka
kuitumia kufanya maandamano hayo inatumika na watu wengi hivyo
nilishughulikia mara moja kuzuia maandamano hayo.
Kamanda
Siro ambaye pia ni Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
alitoa madai hayo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi
Janeth Kaluyenda.
Upande
wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka
akisaidiana na Salum Mohamed Inspekta wa Polisi Jackson Chidunda.
Akiongozwa
na Kweka, shahidi huyo alidai kuwa Oktoba 2, mwaka huu alipokea barua
iliyopitia kwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,
kutoka Bawacha wakiomba kufanya maandamani ya amani kwenda Ikulu.
“Katika
barua hiyo Bawacha waliomba kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa Rais
Jakaya Kikwete kumtaka asipokee katiba inayopendekezwa… maandamano hayo
yalipangwa kufanyika Oktoba 4, mwaka 2014 saa 3:00 asubuhi”alidai
Kamanda Siro.
Akifafanua
zaidi alidai kuwa "niwaagiza wafuasi wangu kwenda kukagua njia
waliyotaka kuitumia lakini kwa bahati mbaya haikuwa salama kwa sababu
ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani".
Alidai
kuwa kwa nafasi yake anasimamia vikosi vyote vya kupambana na uhalifu
kwa Kanda Maalum, kwa hiyo nilishughulikia mara moja kwa kuwajibu
Bawacha kwamba maandamano hayo yasifanyike kwa sababu za vigezo vya
kiusalama.
Aidha,
Kamanda Siro aliomba mahakama ipokee nakala ya barua hiyo kama
kielelezo lakini yalitokea mabishano ya kisheria na kesi hiyo
imeahirishwa hadi Machi 3, mwaka huu ushahidi utakapoendelea
kusikilizwa.
Mbali
na Mdee, washtakiwa wengine ni,Rose Moshi , Renina Peter maarufu kama
Lufyagila, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fangel, Edward Julius,
Martha Mtiko na Beatu Mmari.
Katika
kesi ya msingi, washitakiwa hao wanadaiwa Oktoba 4,mwaka 2014, katika
mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika
iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi Emmanuel Tille kwa niaba ya Jeshi la
Polisi.
Pia wanadaiwa siku hiyo walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo moja la kutembea kwenda ofisi ya Rais Kikwete.
0 comments :
Post a Comment