INAENDELEA HAPA:
Baada ya kuvutana sana kati ya Mwalimu mkuu na Mr.
Brown ofisini ikabidi mwalimu mkuu akubali kuwa mpole na kurudisha pesa
japo sio zote ilibidi mwalimu mkuu atoe nusu ya pesa zilizolipwa, Mr.
Brown alilipa ada Shilingi laki moja na nusu ikabidi mwalimu mkuu atoe
nusu ya pesa hizi Shilingi elfu sabini na tano na kumpa Mr. Brown. Mr.
Brown akapokea zile pesa Shilingi elfu Sabini na tano akamchukua binti
yake JENIFER wakaondoka na kuelekea nyumbani kipindi wapo njiani
wanaelekea nyumbani, Mr. Brown alikua na hasira sana akamwambia binti
yake JENIFER "We mtoto leo tukifika tu nyumbani chukua nguo zako na
uondoke nyumbani kwangu sitaki kukuona, mshenzi wewe!". Walipofika
nyumbani tu Mr. Brown akaanza kumuhadithia mke wake Mrs. Brown
yaliyotokea shuleni kuhusu binti yao JENIFER na akamwambia Mrs. Brown
kuwa hataki hata kumuona aondoke nyumbani kwake lakini kwa maamuzi haya
ya Mr. Brown mke wake Mrs. Brown hakuafikiana nayo akamwambia mume wake
"SASA MUME WANGU UNAMFUKUZA MTOTO AENDE WAPI WAKATI
HAPA NDIO KWAO, UNADHANI ATAENDA WAPI? KAMA MAJI YAMEISHAMWAGIKA MAKOSA
NDIO KISHAFANYA HAKUNA JINSI NI KUMSAMEHE NA TUKAE TUSHAURIANE TUJUE
TUNAFANYAJE MUME WANGU PUNGUZA HASIRA". Mr. Brown akamjibu "HAIWEZEKANI
MIMI SITAKI HATA KUMUONA HUMU NDANI AONDOKE SITAKI KUMUONA". Mrs. Brown
nae akamjibu "KAMA UNATAKA HUYU BINTI AONDOKE HUMU NDANI BASI JUA
NITAONDOKA NAE SIWEZI KUKUBALI BINTI YANGU AONDOKE AKAPATE SHIDA WAKATI
KWAO ANAPO, UKIMFUKUZA JUA NAMIMI NAONDOKA HUMU NDANI" Baada ya Mrs.
Brown kumuambia Mume wake Mr. Brown maneno hayo ghafla Mr. Brown alisema
kwa sauti kali ya juu "SAWA MKITAKA MUONDOKE WOTE, SIWEZI KUFUGA
UPUMBAVU KAMA UNAONA NAMUONEA MTOTO WAKO MFUATE MUONDOKE WOTE PUMBAVU!".
Mrs Brown akamjibu "EH E! TAFADHALI BABA WEE, USINITUKANE NGOJA
TUKUPISHE UBAKIE NA NYUMBA YAKO SIO UNIFOKEE. MPUMBAVU MWENYEWE!. Ghafla
Mr. Brown alikurupuka na kumvamia mke wake Mrs. Brown na kuanza kumpiga
makofi huku akimwambia
"YANI WEWE UNADIRIKI KUNIAMBIA MIMI MPUMBAVU, WAKATI
JENIFER KAFANYA MAKOSA DHAHIRI. HIVI MIMI NINAVYOHANGAIKA KUTAFUTA PESA
ZA KUMSOMESHA HALAFU ANALETA UPUMBAVU UNAFURAHIA ETI EEH!"
0 comments :
Post a Comment