MBUNGE
wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeish Hilaly amesema hatajiuzulu ng’o nafasi
yake kama Mbunge kwa sababu za CCM kushindwa vibaya katika uchaguzi wa
marudio uliofanyika juzi katika kata tatu na mitaa miwili wilaya ya
Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa.
Uchaguzi
huo uliofanyika katika kata za Msua ,Kizwite na Chanji pamoja na mitaa
miwili ya Bangwe kata ya Izia na Tambazi kata ya Sumbawanga mjini,
ulikuwa wa marudio baada ya kuahirishwa kufanyika Desemba 14 , mwaka
jana.
Uchaguzi
uliokuwa ufanyike Desemba 14 mwaka jana , katika kata hizo uliahirishwa
kutokana na kasoro mbalimbali na kusababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa
halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, William Shimwela kusimamishwa
kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake ufanyike.
Alisema
licha ya CCM kufanya vibaya katika uchaguzi wa marudio bado CCM ina
matumaini na nafasi kubwa ya kushinda kwa nafasi za udiwani , ubunge na
urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
0 comments :
Post a Comment