Khadija Kopa,
ni mwanamuziki wa Taarab mwenye jina kubwa sanaa hapa nchini Tanzania
na mbaye alikuwepo katika show moja iliyofanyika Dar na kukatokea
tafrani za wasanii kurushiwa makopo wakiwa jukwaani.
Khadija Kopa amesema hakupendezwa na tukio hilo kwa kuwa inawavunja moyo wasanii wetu hao ambao ni wawakilishi wetu wa nchi.
KUHUSU BIFU LA DIAMOND NA KIBA
Malkia huyu wa Mipasho alizungumzia pia mastaa wawili wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Diamond na Ali Kiba akasema
kama kuna hali ya kutokuwa na maelewano kati yao ni vizuri wakakaa na
kumaliza tofauti zao kwa kuwa hata yeye na marehemu Nasma Khamis Kidogo walikuwa marafiki ila mashabiki ndio walikuwa wanarushiana vijembe kupitia nyimbo zao.
akasema
kuwa mashabiki wamekuwa ni watu ambao wanatengeneza bifu zao huko
mitaani kwao kulingana na mapenzi yao kwa wanamuziki hao, lakini kumbe
huku waliko wanapatana na pengine hata kuchangiana mawazo ya kikazi
0 comments :
Post a Comment