Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha
marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa
sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.
"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa nyumbani amekaa
lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye kidogo alifariki" amesema Jerry
Komba mtoto wa marehemu.
Marehemu Kapteni John Komba |
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
0 comments :
Post a Comment