UTAMU WA PILIPLI HOHO
≡
Navigation
Home
HABARI
WASANII
SPORTS
FOOTBALL
MPIRA WA MIGUU
BASKETBALL
LOVE
LOVE
MAPENZI
SIASA
GOSSIP
Download This Template
Home
»
MAPENZI
» JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 2
JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 2
Written By MWAYANGASPORTS on Sunday, 8 March 2015 | 17:33
INAENDELEA HAPA:
Baada ya JENIFER na wenzake kukamatwa na mwalimu na kupewa adhabu hiyo ya kwenda na wazazi wao shuleni siku ya Ijumaa tatu na kupelekea kupoteza mudi ya kuendelea kufurah usiku huo ikawabidi waondoke kabisa sehemu hiyo ya CLUB usiku huo huo na kwenda kulala kwenye chumba cha rafiki yao CHRISTINA waliekuwa nae katika kundi lao usiku huo, ilipofika kesho yake siku ya ijumaa pili asubuhi kila mtu alirejea nyumbani kwao huku wakiwa na sura za hudhuni na mawazo kibao kichwani wakijiuliza itakuaje kesho yake ambayo ni siku ya Ijumaa tatu wanatakiwa waende shule na wazazi wao?!. Jenifer alipofika kwao moja kwa moja alielekea chumbani kwake na kujilaza kitandani huku akiwa na mawazo kibao hata chakula hakuweza kula siku hiyo muda wote alikua kajifungia chumbani analia. Ghafla akasikia mlango wa chumbani kwake unafunguliwa aliposhtuka akamuona mama yake Mrs. Brown. Mrs. Brown alimsogelea binti yake Jenifer kuanza kuzungumza nae kama ifuatavyo:-
MRS. BROWN:
"Jenifer binti yangu mbona unaonekana leo hauko sawa, nini tatizo mwanangu?! Na mbona unalia?
JENIFER:
"Hapana mama, wala usijali hamna kitu chochote naomba uwe na amani mama yangu, niko sawa tu!"
MRS. BROWN:
"Jenifer mwanangu lazima kutakuwa kuna kitu ila unaficha. Mwanangu nakuomba unieleze usinifiche niambie tu mwanangu wala usiogope"
JENIFER:
"Mama wala usijali hakuna kitu chochote kile"
MRS. BROWN:
"Sidhani binti yangu kama kweli hakuna tatizo sasa mbona unalia, Au umepata ujauzito?!
JENIFER:
"Mama bora ningekua nina ujauzito ila kwa hiki kilichonipata mama yangu najuta tena najuta hata sijui kwanini mlinipeleka shule mama yangu"
MRS. BROWN:
"Mwanangu mbona unasema hivyo kwani kuna tatizo limetokea shule?!
JENIFER:
"Ndio mama, kuna mwalimu shuleni alinitongoza nikamkatalia sasa kila siku huwa ananichapa fimbo bila makosa na ananitesa sana shule na kaniahidi kuwa atanitafutia kosa lolote la uongo ili nifukuzwe shule anikomoe na juzi siku ya Ijumaa kuna wanafunzi kawakamata usiku CLUB akawaambia kuwa atawafukuza shule sasa kaniambia namimi ataniingiza katika hilo kosa la hao wanafunzi kesho shuleni ili nifukuzwe namimi"
MRS. BROWN:
"Haiwezekani mwanangu wewe nyamaza acha kulia tumsubiri baba yako aje nimuelezee ikiwezekana kesho akupeleke shule akamkomeshe huyo mwalimu, wala usiwaze sana mwanangu Jenifer looooo, huyo mwalimu hana hata aibu"
Baada ya Jenifer kutumia uongo wa kumdanganya mama yake Mrs. Brown kwa dhumuni la kujitetea kutokana na kosa alilolifanya usiku wa jana yake walipokutwa na mwalimu wao wa shule CLUB ikamlazimu kumpa kesi ya uongo yule mwalimu kwa wazazi wake ili wasimuone yeye anamakosa. Mama yake na Jenifer Mrs. Brown alihamaki na kuingiwa na hasira akawa anamsubiria mume wake arudi ili amuelezee kilichotokea. Ghafla baba yake na Jenifer Mr. Brown akaingia nyumbani kwake na kumkuta mke wake Mrs. Brown akiwa na binti yao Jenifer, Jenifer alipomuona baba yake Mr. Brown akaanza kuangua kilio huku akisema "BABA NAJUTA MIMI MWANAOO, NAJUTA BABA HIVI KWANINI ULINIPELEKA NIKASOME ILE SHULE BABA YANGUUUUUU" Jenifer alikua analia huku akitoa sauti kubwa ya kumlalamikia baba yake. Mr. Brown alipigwa na butwaa hakujua nini kinachoendelea ikabidi akae chini na kumuuliza mke wake "MKE WANGU NINI KIMEMPATA BINTI YETU JENIFER?" Mrs. Brown akamjibu mume wake "MUME WANGU NENDA KWANZA KAKOGE KISHA ULE HALAFU NDIO NIKUELEZEE KILICHOTOKEA" Mr. Brown nae akamjibu "HAPANA MKE WANGU NIELEZEE KWANZA NIJUE TATIZO NINI?". Mrs. Brown ikabidi aanze kumuhadithia kama alivyohadithiwa na binti yao Jenifer kuwa kuna mwalimu wa shule alimtongoza binti yao akamkataa sasa huyo mwalimu anamtesa sana Jenifer shuleni na kamuahidi atamfanyia njama yoyote ili binti yao afukuzwe shuleni. Pale pale Mr. Brown nayeye akapandwa na hasira akamnyamazisha binti yake Jenifer na kumwambia "JENIFER BINTI YANGU NYAMAZA, KESHO IJUMAA TATU ASUBUHI TUTAKWENDA WOTE MPAKA SHULENI KWENU UKANIONESHE HUYO MWALIMU. ATANITAMBUA" baada ya hapo wakatawanyika Jenifer akaingia chumbani akaanza kushangilia peke yake kimya kimya akiwa na imani kuwa kishamaliza kesi aliyokuwa nayo na akawa na furaha tele akaendelea kufanya mambo yake kama kawaida.
SHARE
SHARE
SHARE
About MWAYANGASPORTS
RELATED POSTS
0 comments :
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Popular Posts
JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 4
INAENDELEA HAPA: Mwalimu KABAVAKO aliwachapa kila mmoja fimbo nne nne, kisha akawarudisha ofisini kwa mwalimu mkuu walipofika ofisini...
Anataka kunifanya usiku mzima, kwasababu nina matako mkubwa na mapaja mkubwa, matiti madogo
Mimi nina rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki baada ya kuajiriwa siku moja hapa jijini! Kwa kweli, bila hata kumaliza mwenzi mmoj...
JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 2
INAENDELEA HAPA: Baada ya JENIFER na wenzake kukamatwa na mwalimu na kupewa adhabu hiyo ya kwenda na wazazi wao shuleni siku ya Ijuma...
JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI" PART 1
AMANI MIE UKAHABA SASA BASI ni Hadithi inayomuhusu binti wa kitanzania alietunukiwa uzuri wa asili na mvuto wa kipekee aliojaaliwa na...
HIZI NDIO SEHEMU NYETI 12 ZINAZOMPA MWANAMKE RAHA KATIKA MAPENZI:
Tendo la ndoa au ngono ndilo tendo la furaha lililo kuu kwa binadamu. Wakati tendo hilo kwa wanyama lipo kwa ajili ya kuzaa,kwa upand...
Am 29 Years but Can't Seem To Get a Man.....Please Sample My Pics and Help Me Get One!!!!
A girl in Facebook went on to post her desperate hunt for a hubby before she pulled the post and profile off.. See the photos she pos...
No More Twerking!!, Tanzania Bans The Provocative Dance
“This sounds like violation of human rights? You have a bum but you can’t put it in use!! Why?? You will provoke weak men to rape...
NEVER marry a SECRETARY
Secretaries play an imperative role in any organisation. They are responsible for the smooth running of the secretarial and clerical...
Never marry a Nairobi waitress
About 80% of the waitresses I have seen in several happening places are hot. They ooze sex all the way and a mere glance at them can...
Top 10 red flags women look for
When it comes to dating, women often go against their better judgement and overlook quirky things men do to cut them some slack. Althou...
Follow via Facebook
Follow via Twitter
Follow via Google
Follow via Pinterest
Follow via Youtube
Follow via RSS
0 comments :
Post a Comment