Home » » Mwigizaji Dokii Ajipumzisha Kwa Kocha wa Yanga..Mwenyewe Asema Haya

Mwigizaji Dokii Ajipumzisha Kwa Kocha wa Yanga..Mwenyewe Asema Haya

Written By MWAYANGASPORTS on Monday, 9 March 2015 | 10:09

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameanzisha urafiki wa karibu sana na Kocha wa Timu ya Yanga, Hans van der Pluijm, Raia wa Uholanzi.
Ukaribu wa Dokii na kocha huyo ulichipukia kwa kasi Januari, mwaka huu walipokutana katika Kombe la Mapinduzi, Zanzibar kisha kuzidi kuwasiliana kwa ukaribu hadi kuwafanya wapenda ‘ubuyu’ wautilie mashaka.

Alipotafutwa Dokii ili aweze kuufafanua zaidi ukaribu wao kama umejiongeza zaidi na kuwa wapenzi, alijibu kwa kifupi tu pasipo kufafanua zaidi.“Hakuna tatizo mimi kuwa naye karibu, namkubali na yeye ananikubali pia. Ni mshkaji sana jamaa.”
Kocha huyo hakupatikana hewani alipotafutwa lakini jitihada zinaendelea
SHARE

About MWAYANGASPORTS

0 comments :

Post a Comment