Home » » Ndege ya kwanza inayotumia Nishati ya Jua yazinduliwa

Ndege ya kwanza inayotumia Nishati ya Jua yazinduliwa

Written By MWAYANGASPORTS on Monday, 9 March 2015 | 10:10

Jaribio la kwanza la ndege inayotumia umeme jua limefanyika leo baada ya ndege hiyo kufanikiwa kuanza kuruka asubuhi ya leo.
Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi.
Ndege hiyo yenye kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa wa jumbo jet huku ndege yenyewe ikiwa na uzito sawa na gari, mabawa yake yamefunikwa na vifaa vya vya kunasia mionzi ya jua yaani solar panels.


Betri zake zina uwezo wa kuhifadhi nguvu ya umeme jua kutoka kwenye jua na hivyo kuiweza kusafiri hata nyakati za usiku.
Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao.
SHARE

About MWAYANGASPORTS

0 comments :

Post a Comment