Home » » RECHO APIGA MWEREKA KATIKATI YA SHEREHE

RECHO APIGA MWEREKA KATIKATI YA SHEREHE

Written By MWAYANGASPORTS on Sunday, 1 March 2015 | 17:19

 
MREMBO kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’, amepiga mwereka wa aina yake baada ya kuteleza ukumbini, Risasi Jumamosi limeshuhudia.
Tukio hilo lilijiri juzikati katika Hoteli ya Regence, Mikocheni jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (bethidei).
Mrembo kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’.
Wakati sherehe ikipamba moto, wageni waalikwa walimmwagia Recho maji na mvinyo kama ishara ya upendo na kusababisha sehemu aliyokuwa amekaa kutapakaa maji.
Wakati zoezi la kummwagia maji na mvinyo likiendelea, katikati ya sherehe, mwanahabari wetu aliyekuwepo ukumbini hapo, alishuhudia mrembo huyo akiteleza na kuanguka chini ambapo wenzake hao hawakujali, wakaendelea kummwagia hali iliyosababisha msanii huyo aangue kilio.
Recho akiwa chini baada ya kupiga mweleka.
“Jamani inatosha, muoneeni huruma kidogo hii sasa si sherehe tena hapa mnamsulubu,” alisikika mmoja wa waalikwa.
Baadaye wageni waalikwa walimfuta Recho maji na zoezi la kukata keki na kulishana kwa ‘staili ya njiwa’ likaendelea huku waalikwa wakiendelea kukata ulabu.
Recho akisadiwa kunyanyuka.
Baada ya shamrashamra kutulia, mwanahabari wetu alimvuta pembeni Recho na kutaka azungumzie sherehe hiyo ambayo katikati ilimfanya aangue kilio: “Nimejikuta tu nikilia na hasa sikutegemea kama wangenimwagia pombe na maji kiasi kile, nywele nilizoweka kichwani zinaniuma sana lakini pia pombe ziliniingia machoni, kimsingi ni jambo la furaha lakini ndiyo hivyo limeniliza,” alisema Recho.
Sherehe hiyo iliwakusanya waalikwa mbalimbali akiwemo shosti yake Recho wa damu, staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga ‘Linnah’.

SHARE

About MWAYANGASPORTS

0 comments :

Post a Comment