Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetahadharishwa kisifanye mzaha na uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, kwani kisipoteua mtu makini na mchapa kazi anayekubalika na jamii, mgombea atakayesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), atashinda kirahisi urais uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
kwenye mazishi ya kada maarufu wa CCM wilayani Kahama, Emmanuel Chupa,
Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Nyasubi,
Leonard Mayala, alisema ana amini chama hicho kitakosea iwapo
hakitampitisha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwania urais, ambaye anaonekana ana nguvu ndani ya chama hicho na ataisumbua Ukawa katika uchaguzi mkuu ujao.
Alisema
kwa hali ya kisiasa inavyoonekana nchini kwa sasa, ni wazi Watanzania
wanahitaji Rais ajaye awe mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi na uzoefu
katika masuala ya uongozi na kiutawala na si kuchagua kiongozi wa kwenda
kujifunza kufanya kazi Ikulu.
Hata
hivyo, alisema imani yake ni CCM itateleza katika uteuzi wake na kuteua
mgombea asiyekubalika kwa Watanzania wengi, hivyo kutoa nafasi kwa
Ukawa kuongoza nchi.
“Licha
ya mimi kutoka kambi ya upinzani, lakini na amini Lowassa akiteuliwa na
CCM atasukuma kasi ya maendeleo na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na
uchumi wa taifa kwa ujumla,” alisema.
0 comments :
Post a Comment