Afisa Elimu ya mpiga kura na
Elimu kwa umma kutoka tume ya Uchaguzi(NEC), Salvatory Alute akitoa mada kwenye
mdahalo wa Vyuo vikuu Mbeya.
Joseph
Mallya kutoka Idara ya daftari la kudumu la mpiga kura akiwasilisha mada yake
kwenye mdahalo wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu Mbeya uliofanyika katika ukumbi
wa TEKU.
|
Baadhi ya waratibu wa mdahalo huo wakichukua dondoo. |
Walimu
wa TEKU wakifuatilia hoja mbali mbali katika mdahalo.
|
Washiriki
wa mdahalo huo kutoka vyuo mbali mbali vya Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa
makini.
|
WAKATI
zoezi la uandikishaji wa Wapiga kura katika daftari la Kudumu likiwa limeanza
Makambako Mkoani Njombe, Wasomi wa Vyuo vikuu Mkoa wa Mbeya wameonesha
hofu ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
Wakizungumza
na kwenye mdahalo wa vyuo vikuu uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa
Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) ulioandaliwa na Chama cha walimu
wanaofundisha masomo ya Siasa(CETA), walisema ratiba ya uchaguzi si rafiki kwa
wanafunzi.
Nurdin
Makoni, Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa TEKU alisema masharti yaliyowekwa
na Tume ya uchaguzi kwamba ni lazima kila mtu apige kura katika eneo
alilojiandikishia linawabagua wanafunzi kutokana na muda wa uchaguzi kuwa eneo
tofauti na alipojiandikishia.
Alisema
asilimia kubwa ya wanafunzi hujiandikisha aidha akiwa chuoni ama nyumbani
lakini siku ya uchaguzi huenda akawa sehemu tofauti na alipojiandikishia jambo
ambalo linamnyima haki yake ya kupiga kura na kuchagua viongozi.
Frank
David mwanafunzi wa Chuo kikuu Mzumbe alisema miaka mingi ya uchaguzi idadi ya
wapiga kura inakuwa hairidhishi kutokana na kuwabagua vijana kwa sababu ya
ratiba ambayo si rafiki kwa wanafunzi walioko vyuoni ambao ndiyo wengi zaidi
kuliko watu wengine.
Alisema
Tume inapaswa kuwa wazi kwa vijana na wanafunzi walioko mashuleni ili
wawe huru kuchagua viongozi wao kwa kuweka ratiba na maeneo ambayo wanapaswa
kupigia kura katika uchaguzi mkuu ujao na kutopoteza haki yao.
Naye
Frida Kitika kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii alisema ni vema wanafunzi
wakapewa uhuru wa kupiga kura sehemu yoyote watakapo kuwepo ili wasiwanyime
haki ya kuchagua viongozi wao kutokana na mazingira wanayoishi kuwa si ya
kudumu.
Alisema
Changamoto nyingine inatokana na wengi wao kutofikisha umri wa miaka 18 kabla
ya kuanza chuo lakini hufanikiwa kufikisha miaka inayotakiwa tayari akiwa
ameanza masomo hivyo kusababisha kukosa sifa ya kuchagua viongozi wake.
Wanafunzi
hao walishauri kuwa endapo tume itaendelea kusimamia msimamo wake ni bora
wanafunzi wakawekewa utaratibu wa kumchagua Rais kwa kuwa ni kiongozi wa
kitaifa tofauti na Wabunge na madiwani ambao wanapaswa kuchaguliwa na wakazi wa
eneo husika.
Kwa
upande wake Afisa Elimu ya mpiga kura na elimu kwa umma kutoka tume ya
uchaguzi, Salvatory Alute,alisema ni vema vijana wakajitokeza kujiandikisha
kwenye daftari la kudumu bila kuhofia ni wapi watakapokuwepo siku ya uchagfuzi.
Alisema
zoezi la kujiandikisha ni muhimu kutokana na kutolewa vitambulisho vipya
tofauti na ambavyo tayari vipo kwa walioandikishwa zamani na kushiriki chaguzi
zilizopita.
Alisema
Tume imejipanga kuhakikisha zoezi la uandikishaji linafanyika katika kipindi
kifupi kutokana na vituo kuongezwa kutoka vituo 23000 hadi vituo 40000 smbsvyo
vitakuwepo kila kijiji ili kurahisisha wananchi wengi kujiandikisha.
Alisema
Serikali imetoa vifaa zaidi ya 8000 ambavyo Tume itakuwa ikivitumia ambapo
itafanya mtindo wa kuhama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine na kutoruhusi
zoezi hilo kuendeshwa kila sehemu hivyo kila Wilaya Daftari litakuwepo kwa siku
28.
Aliongeza
kuwa mfumo utakaotumika kuandikishia ni wa kisasa unaojulikana kwa jina la BVR
ambao umeonesha mafanikio makubwa katika nchi za Kenya na Ghana hivyo Tume
inatarajia kuandikisha watu zaidi ya Milioni 22.
Katika
mdahalo huo zaidi ya wanafunzxi 100 walihudhuri kutoka vyuo vilivyo na matawi
Mbeya ambavyo ni Mzumbe, Iringa, Chuo kikuu kishirki(OUT), TIA, MUST,, VETA,
St. John Nursing, Dar cit college, Tanzania social studies, TEKU, Maendeleo ya
Jamii, CBE, SAUT na Chuo cha Kilimo Uyole.
0 comments :
Post a Comment