Mgeni rasmi katika mashindano ya safari lager
nyama choma, Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela, akizungumza na
wakazi wa Jiji la Mbeya kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Meneja wa Bia ya Safari lager Edith Bebwa, akitoa neno la utangulizi kabla ya kuanza kukabidhi zawadi katika fainali ya nyama choma. |
Mgeni rasmi akiwa meza kuu pamoja na uongozi wa TBL. |
Jaji Mkuu akitaja majina ya washindi |
Mgeni rasmi pamoja na watumishi wa TBL
wakijiandaa kuanza kutoa zawadi.
|
Mwakilishi wa mshindi wa kwanza ambaye ni Tumain
Bar akionesha kombe juu.
|
Picha ya pamoja washindi wote pamoja na uongozi. |
Baadhi ya washindi wakipokea zawadi kutoka kwa
mgeni rasmi.
|
Meneja wa bia ya safari pamoja na mkuu wa
matukio Kanda wakifuatilia kwa makini mashindano ya kuchoma nyama.
|
Watumishi wa TBL wakila nyama kwenye moja ya mabanda ya mashindano |
Pilikapilika kwenye mabanda ya mashindano ya
nyama choma zikiendelea.
|
Wateja mbali mbali wakiwa wanapata huduma kwenye mabanda. |
Watazamaji wakifuatilia mashindano.
|
. Band ya Baby TOT ikitoa burudani. |
. Majaji wakiendelea na kazi.
|
Wananchi mbali mbali waliojitokeza wakifuatilia mashindano. |
Eneo la viwanja vya TIA likiwa limepambwa na
mabango ya safari lager.
|
BAA ya Tumain iliyopo Ilomba jijini Mbeya
imeibuka kinara wa kuchoma nyama katika Fainali iliyofanyika jana kwenye
viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA).
Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya
Bia Tanzania(TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari yaliyojulikana kwa jina la
Safari lager nyama choma 2015 yalishirikisha baa zaidi ya 20 ambapo baa tano
zilitinga fainali.
Mshindi wa kwanza katika fainali hizo Baa ya
Tumaini ilijinyakulia Kombe kubwa,Fedha taslimu shilingi Milioni Moja pamoja na
Cheti maalumu.
Jaji Mkuu wa Mashindano hayo, Manase alisema
mshindi amepatikana kutokana na vigezo ambavyo waliambiwa kwenye semina elekezi
kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na usafi
wa mazingira yanayochomewa nyama, usafi wa mchomaji mwenyewe,aina ya nyama
anayopaswa kuchoma, mazingira kwa ujumla pamoja na utoaji huduma kwa wateja.
Aliitaja baa iliyoibuka msindi wa pili kuwa ni
City Pub iliyopo Mwanjelwa iliyojipatia Cheti na fedha shiliki Laki nane,
mshindi wa tatu Kalembo baa ya Sokomatola iliyojipatia cheti na shilingi laki
sita, msindi wa nne ni Samaki samaki aliyoibuka na Cheti pamoja na
shilingi laki nne huku nafasi ya tano ikienda kwa Nebana baa iliyopata
Cheti na shilingi laki mbili.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika fainali hizo,
Quip Mbeyela Katibu tawala Wilaya ya Mbeya, aliipongeza Kampuni ya Bia
TBL kuwa imekuwa ikijitahidi kushirikiana na serikali katika kutoa huduma na
kuwawezesha wajasiliamali wadogo.
Aliongeza kuwa pia Kampuni hiyo imekuwa
mstari wa mbele katika kulipa Kodi ambayo imekuwa ikiisaidia Serikali katika
kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa jamii.
Naye Meneja wa Bia Safari lager nchini, Edith
Bebwa alisema fainali hizo zimeanzia mkoani Mbeya kutokana na wakazi wa Mkoa
huo kuongoza katika Unywaji wa bia ya Safari.
Alisema baada ya hapo zoezi hilo litahamia
katika mikoa mingine na kuongeza kuwa lengo la mashindano ni kuwawezesha walaji
wa nyama wanapata kitu ambacho kimeandaliwa katika mazingira sahihi.
0 comments :
Post a Comment