Wakati hit single ya Diamond Platnumz, Ntampata Wapi inatoka mwaka
jana, watu wengi waliamini kuwa wimbo huo amemwandikia ex wake, Wema
Sepetu.
Tetesi hizo zilienea baada ya kubainika kuwa wawili hao wameachana tena. Hata hivyo Wema amedai kuwa si kweli.
“Leo nasema rasmi kuwa hii nyimbo hakuniandikia mimi,” Wema aliiambia Radio 5 ya jijini Arusha.
“Because nilikuwa naisikia hii nyimbo hata wakati tulipokuwa kwenye
uhusiano amekuwa akiimba, akiindika kwahiyo ilikuwa tu ni moja ya nyimbo
zake kama anavyoandika nyimbo zote lakini nadhani tu timing ya kutoka
ndio kidogo imekuwa na utata because kaitoa timing ambayo watu wote
wakadhani kamuimbia Wema but in real sense noo,” aliongeza Wema.
0 comments :
Post a Comment