![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4pZNvKW4zUv9udKLDWuhyJ7rhHdxC5VDEFzaH4XxXN0YLOUbhYTcCQVZf7ngPPZkF8EEKy64KjzysE-f94W0V4eIL11L3yf8LweBWpGsuOX8e4ici88K1vPnb3OARr5RJPmqlbWKYmHg/s640/1.jpg)
Hapa kwetu Tanzania habari ya
kubambakiziana kesi ni kama mtindo. Mara nyingi matendo haya yamekuwa
yakifanywa na watu wenye uwezo kifedha
dhidi ya wasio na fedha pia kati ya maofisa wa polisi na
raia.
Mtu kwasababu ana pesa au cheo anaweza kuamua kumfungulia yeyote mashtaka. Watu wengi wako magerezani kwa kubambikizwa kesi, hili wala sio siri tena.
Sisemi walio mahabusu, hao nao hawana idadi. Inasikitisha mno. Ni wazi kuwa wengi wao wamefikia huko aidha kwa kusingiziwa kosa na askari au mtu mwenye cheo au fedha.
Lakini zaidi wametoka mikononi mwa askari kwakuwa hata huyo mwenye cheo au fedha hawezi kumbambikizia mtu kesi bila kupitia kwa askari. Kwahiyo askari ndio tatizo kubwa katika hili.

1.Nini maana ya kubambikizwa kesi.
Kubambikizwa kesi au
kumshtaki mtu kwa hila maana yake ni kumfungulia mtu kesi ya jinai bila mafanikio , na
bila sababu za msingi za kufanya hivyo na mtu huyo akapata athari zozote kutokana na kumfungulia kesi
hiyo.
Athari ni pamoja na kupotezewa muda, gharama, usumbufu, kudhalilishwa, kupata hasara kibiashara au kikazi kutokana na kushikiliwa na kila kitu ambacho kimekuwa kama matokeo ya kusingiziwa kesi ni athari kwa maana hii.

2. Sababu za kuwabambikiza watu kesi.
Sababu za kumuuzia mtu kesi huwa ni nyingi. Ni nyingi
kutokana na kuwa kila
aliyebambikizwa kesi huwa kuna mgogoro nyuma
uliosababisha jambo hilo na migogoro
kawaida inatofautiana.
Pamoja na hayo sababu kuu za kubambikizia mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa au kulipiza kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro kama nilivyosema.
Pamoja na hayo sababu kuu za kubambikizia mtu kesi huwa ni kwa ajili ya kumkomoa au kulipiza kisasi kutokana na chuki zilizotokana na mgogoro kama nilivyosema.
3. Weledi wa Askari wetu na kuwabambikiza raia Kesi.
Wakati mwingine
askari wetu huwabambikizia watu kesi
katika mazingira ya
kushangaza kabisa. Askari
anaweza kumbambikizia raia
kesi kwasababu tu
raia amehoji jambo
fulani.
Kwa mfano mtu anaweza kumuuliza askari nioneshe kitambulisho chako kabla hujanikamata. Utasikia askari akimwambia mtu unajifanya mjuaji tutaona, mara unanifundisha kazi utanitambua n.k.
Eti mazimgira kama hayo kwa askari wetu utakuwa tayari ni mgogoro na mtu atapofikishwa kituoni basi ni rahisi kupewa kesi ambayo si yake ilimradi tu askari aoneshe kuwa aliposema utanitambua, utaona alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo kweli.

4. Athari za kubambikiza watu kesi.
Kwanza upelelezi wa
kesi ambayo haipo unagharimu pesa za
serikali na muda ambao kimsingi ungetumika kushugulikia kesi nyingine za watu
wanaohitaji haki kiukweli.
Pili kesi hizi za kubambikizwa zinaongeza idadi ya kesi mahakamani pasi na sababu za msingi na hivyo kusababisha kesi za kweli kuendelea kuchelewa.
Tatu kesi hizi ni usumbufu kwa waliobambikizwa na ndugu zao na zinaathiri nguvu kazi katika taifa kwani badala ya watu kuendelea na uzalishaji mali hubaki kushughulikia kesi hizi zisizowahusu na baadhi yao kufungwa kabisa na hivyo kupoteza moja kwa moja nguvu kazi katika jamii.

5.Namna ya kumshitaki aliyekubambikiza kesi.
Kushitaki ninakokuongelea hapa
ni kushtaki kwa madai yaani
kumdai aliyekubambikiza kesi akulipe kutokana na tendo hilo ovu. Hivyo hii itakuwa ni kesi
ya madai na hatua zake ni hizi.
( a ) Kwanza
inategemea unataka akulipe shilingi ngapi. Kuanzia shilingi
moja mpaka milioni
tano utaenda mahakama ya mwanzo. Ukifika hapo mahakamani utaeleza shida
yako pale na watakusaidia kufungua
kesi hiyo.
Aidha kuanzia milioni tano na kuendelea mahakama unayotakiwa kufungua kesi ni ya wilaya na Mahakama kuu. Napo ukifika mahakamani utaelekezwa utaratibu wa kufungua kesi lakini kwa mahakama hizi ni vema ukamuona mwanasheria kabla ya kwenda mahakamani.

( b )Kwa ajili ya kufungua
shauri hilo utaratibu ni mwepesi kihivyo
na bila shaka baada
ya kufanya hayo
utakuwa umefungua kesi ya kulipwa
kutokana na kubambikizwa.
6.Mambo unayotakiwa kujiandaa nayo ili ushinde kesi ya kubambikizwa..
( a ) Kwanza
hakikisha unatunza makaratasi yote yanayohusu ile
kesi ya jinai
uliyofunguliwa kwa kubambikizwa. Makaratasi( documents) hayo ndiyo
yatakayotumika kuonesha kuwa kweli kesi ya jinai
dhidi yako ilifunguliwa.
( b ) Zingatia sana
kuwa kubambikizwa kesi ni pale
tu unapofunguliwa mashtaka polisi na haijalishi mashtaka
hayo yamefika mahakamani
au hapana. Kitendo cha kufikishwa polisi kwamba umetenda kosa fulani wakati si
kweli tayari umebambikizwa kesi.
( c ) Pia kama
ulibambikizwa kesi ikafika
mpaka mahakamani na ukaachiwa huru hakikisha unapata nakala ya hukumu inayoonesha kuwa uliachiwa huru kwakuwa itakuwa ushahidi
kuwa kesi haikuwa ya kweli na ndio maana
mahakama iliitupilia mbali.
( d ) Tatu jiiandae kuonesha kuwa aliyekufungulia kesi alifanya hivyo bila
sababu za msingi. Yaani ionekane wazi kuwa hapakuwa na sababu zozote za msingi
za kufanya hivyo yaani kukufungulia mashtaka kama hayo.
( e ) Pia andaa ushahidi au mashahidi
ili kuonesha ni kwa kiasi gani
uliathirika kutokana na kubambikizwa kesi ili uweze kupata pesa ulizoomba kulipwa. Kuathirika
au kupata madhara
kunakoongelewa hapa sio lazima ziwe athari za kimwili tu.
Zipo athari kama mtu kuharibiwa hadhi yake katika jamii, athari ya kumharibia mtu sifa njema katika jamii, na athari za kumpotezea mtu mali pamoja na muda kutokana na kesi hiyo.
Aidha athari ya mali na muda inatokana na mtu kuacha kufanya shughuli zake na kuanza kusughulikia kesi hiyo ya uongo. Katika kufanya hivyo ni rahisi mtu kufukuzwa kazi au kupoteza kazi yake kwa namna yoyote ile ikiwa ni pamoja na kumharibia mtu mipango yake mbalimbali ambayo ingeweza kumwingizia kipato. Haya yote yanahesabika ni athari ambapo mtu aliyesababisha atatakiwa kuyafidia.

Na hizo athari si lazima zitokee zote. Hata ikitokea moja kati ya hizi
inatakiwa kufidiwa
( f ) Jambo jingine la
muhimu na la mwisho katika kufungua shauri la kubambikizwa kesi ni kuwa lazima
mashtaka aliyosingiziwa mtu yawe ni ya jinai. Yaani ulisingiziwa kutenda jinai kama kuiba, kubaka, kupiga, kutapeli, kutukana,
kusingiziwa kumiliki silaha, n.k.
Imeandikwa na Bashir Yakub.
bashiryakub@ymail.com, 0784482959, 0714047241
0 comments :
Post a Comment