Balozi wa Marekani nchini Korea
Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake
na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa
kipande cha ardhi ya jumuiya yao.
Mara tu baada ya shambulio hilo
Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake
wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya
shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.
Balozi huyo
mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa
upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha
yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na
sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini
kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa
kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo
hicho kwa nguvu zote .
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi
walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu
chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo
mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na
mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini
Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema
kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio
hilo na masuala mengine kumhusu .
Naye msemaji wa baraza la
maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye muandaaji wa mkutano huo,
ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti .
Balozi Lippert,
ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na mambaye pia aliwahi kuwa
msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na bara la
Asia,na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October mwaka
wa jana.
Lippert amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama
wa taifa katika paresheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba
nyeusi wakati alipoitembelea Iraq.
Korea Kusini na Kaskazini
walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya Korea nab ado kiufundi
wako vitani kwakuwa mapigano yalisitishwa kwa suluhu .
Marekani
na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika
mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko
Kaskazini .
Pyongyang wanadai kuwa wana fanya mazoezi kwa kujiweka
tayari na uvamizi wowote utakao tokea wakati huo huo Korea Kusini na
Marekani wao wanadai kuwa mazoezi yao ni kwa kujihami tu .
Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao30,000 vya kudumu vilivyopiga kambi Korea Kusini.
Mark Lippert (katikati) akiwa anajifuta damu
Kim Ki-Jong akiwa amekamatwa na polisi
Mark Lippert akisaidiwa kunyanyuka baada ya kuchomwa na kisu
0 comments :
Post a Comment