Home » » Dr. Wilbrod Slaa Amlilia Marehemu Kapteni John Komba.....Asema Taifa Limepoteza Mpigani wa Kweli!!

Dr. Wilbrod Slaa Amlilia Marehemu Kapteni John Komba.....Asema Taifa Limepoteza Mpigani wa Kweli!!

Written By MWAYANGASPORTS on Sunday, 1 March 2015 | 04:43

 
Yakiwa  Yamepita  Masaa Machache  baada ya Mbunge wa Mbinga mashariki Kaptain John Komba kufariki dunia Gafla kutokana na kusumbuliwa na Ugonjwa wa kisukari kwa mda mrefu, Viongozi mbalimbali wakimwemo wanasiasa wametoa masikitiko yao kufuatia kifo hicho.
 
Wakizungumza na Mpekuzi, wanasiasa hao wameonyesha kugushwa na msiba huo na wa kwanza kuzungumza na mwandishi wetu ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dokta Wilbroad Slaa ambaye amesema kwa kifupi kuwa  yeye mwenyewe amezipata taarifa hizi kupitia mitandao  ya kijaamii na ni taarifa ambazo zimemsikitisha sana. 
 
“Kikukweli mimi mwenyewe nimepata taarifa hizi kwenye mitandao mbalimbali, cha kwanza imenisikitisha sana kwani Komba ni miongoni mwa wanasiasa waliolijenga taifa hili changa kwa mafanikioa makubwa sana” amesema Dokta Slaa. 
 
Dokta Slaa ameongeza kuwa  anatumia nafasi hii kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dr.Jakaya Kikwete  ambacho ndicho chama  Komba anatoka kwa msiba huo mkubwa na akawataka kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu. 
 
Naye Mwenyekiti asiyetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini kutoka chama cha ACT-Tanzania, Kadawi Limbu ametoa pole kwa chama cha Mapinduzi CCM kwa msiba huo pamoja na Wasanii kwa ujumla .

SHARE

About MWAYANGASPORTS

0 comments :

Post a Comment