KAMATI
kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM /CC,imewazuia Viongozi wake waliochukua
pesa kwenye Akaunt ya Escrow kutoingia kwenye Vikao vya juu vya Chama
hicho.
Viongozi
waliozuiliwa ni Mbunge wa Muleba kusini Profesa Anne Tibajuka,Mbunge wa
Bariada Magharibi Adrew Chenge pamoja Mbunge wa Sengerema William
Ngeleja ambao wote kwa pamoja waliingiziwa pesa na Mbia wa kampuni ya
IPTL bwana james Rugimalira kupitia Akaunt ya Benki ya Mkombozi.
Akitangaza
Maazimio hayo ya Kamati ya CC yaliyotokana na kikao kilichofanyika kwa
siku moja Mkoani Dar Es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha
Mapinduzi CCM,Nape Nnauye wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
amesema Kamati kuu ya CCM (cc) imelijadili suala hilo kwa makini na
kuwazuia viongozi hao wasiingie kwenye vikao hivyo
Aidha,Kamati
kuu hiyo ya CCM yaani CC imewarushia mzigo Kamati ya Maadili ya chama
hicho kuangalia adhabu ya Makada wake waliotangaza nia mapema kama
walikiuka adhabu waliyopewa ya kufungiwa kwa miezi 12 kwa makada Sita wa
chama hicho walioanza kampeni mapema ya Urais ndani ya chama hicho
kabla ya muda kuanza.
“Kuhusu
makada wetu waliotangaza nia mapema ya kutangaza uongozi mbalimbali
hususani Urais, tumeiachia Kamati ya Maadili kuangalia kama walikiuka
adhabu waliyopewa au hawakukiuka. Kamati hiyo inatakiwa itutoe majibu” amesema Nape.
Alibainisha kuwa Kamati hiyo ya Maadili imeambiwa ianze kazi mara moja na ipeleke majibu kwenye kamati Kuu.
Makada
hao waliokuwa chini ya adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Kilimo na
Ushirika, Stephen Wasira na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Makada
hao walipewa adhabu hiyo ya onyo kali na Kamati Kuu Februari 18, mwaka
jana baada ya kuthibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea
urais kabla ya wakati kinyume na kanuni za uongozi na maadili za CCM
Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).
Vilevile
baada ya kuhojiwa, walithibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili
ndani ya chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani
ya jamii.
Kutokana
na adhabu ya onyo kali makada hao kwa mwaka mzima walikuwa katika hali
ya kuchunguzwa ili kuwasaidia katika jitihada za kujirekebisha.
Vilevile
Chama hicho kimepokea kwa masikitiko Makubwa Msiba wa Mbunge wa Mbinga
Mashariki Kaptain John Komba na kusema ni pengo kubwa sana.
0 comments :
Post a Comment