Msanii wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ amefunguka
kwamba japokuwa alipata maumivu ya moyo baada ya jirani yake kumbaka
mkewe, Mama Maua ameamua kumsamehe.
Akizungumza Global Tv Online, Kingwendu alisema mara nyingi mkewe
alikuwa akimwambia kuhusu jirani huyo kumtongoza lakini akawa anamkatalia
lakini siku hiyo alimvizia na kutimiza azma yake ambapo baada ya hapo
alikimbia mpaka leo hajarudi ila amemsamehe kwa kuwa hata Mungu
anasamehe mara nyingi.
“Mimi nasali sana hivyo nimeamua kumsamehe huyo jamaa kwa sababu hata
Mungu huwa anatusamehe mara nyingi, alishawahi kumtuma dada yake aje
kuniomba msamaha maana yeye alikimbilia huko Kilwa na mimi na mke wangu
tuko vizuri ninampenda sana na najua halikuwa kusudi lake ila mwanaume
huyo alimsumbua kwa muda mrefu,” alisema Kingwendu.
0 comments :
Post a Comment