Home
»
MAPENZI
»
MBINU ZA KUDUMU NA STAA KWENYE UHUSIANO!
UMEWAHI
kujiuliza; kwanini mastaa wengi hawadumu na wenzi wao? Nimeamua
kuchambua mada hii kwa sababu tunao mastaa wengi kwenye jamii yetu ambao
wana uhusiano ama na mastaa wenzao au watu wa kawaida.
Pia,
wapo watu ambao wanatarajia kuwa na uhusiano na mastaa, wakati kuna
ambao tayari wapo ndani ya penzi na watu maarufu. Pamoja na hayo yote,
wengi huwa wanashindwa kudumu kwa muda mrefu na mastaa kwa sababu za
hapa na pale.
Katika mada hii ambayo nimeifanyia utafiti wa muda
mrefu, itakufanya mpya katika uamuzi wako, ndani ya uhusiano na staa au
staa ambaye yupo katika uhusiano na mwenzi asiye staa.
Labda tuwekane
sawa kidogo, hapa namzungumzia mtu maarufu katika jamii, maarufu kwa
maana ya kujulikana sana. Ustaa wa mtu unaweza kusababishwa na kazi au
sanaa. Mathalani, sanaa za maigizo, soka, ndondi, riadha, siasa, urembo,
utangazaji, uandishi wa habari, mitindo, utunzi, uchoraji, uchongaji,
biashara nk.
Siwezi kutaja moja kwa moja majina ya mastaa, lakini
naamini nimeeleweka vyema kuwa nawazungumzia watu wa aina gani. Watu
wanaojulikana sana katika jamii kulingana na kazi zao za kila siku.
WASIKIE MASTAA
Wakati
naandaa mada hii, nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya mastaa
ambapo walitoa maoni yao. Kwa bahati mbaya sana, wote niliopata
kuzungumza nao, walipojua mazungumzo yetu yangeishia kuwa mada gazetini
waliomba kuhifadhiwa majina yao.
Hebu wasikilize: “Kiukweli kaka
Shaluwa, naweza kusema sisi wanawake wenyewe ndiyo wenye
matatizo...asikudanganye mtu, ustaa kazi. Ukishakuwa maarufu, unataka
mambo mengi; vipodozi, gari, nguo mpya, kujirusha, simu iwe na full
vocha nk.
“Sasa kama unakuwa na boy ambaye anajifanya anakuchunga
sana, inakuwa ngumu kudumu na sisi tulivyo jeuri, akikuacha asubuhi,
jioni kiwanja unakutana na mwingine.”
Huyu ni staa wa muziki wa dansi nchini kama alivyozungumza nami jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Kiukweli
huwa tunaacha sana mademu, lakini siyo suala la umalaya hapo brother
Shaluwa. Kuna mambo mawili makubwa; kwanza, mwanamke anakuwa anapenda
ustaa wako na siyo penzi la dhati, pili anakubana na kukupangia sana
ratiba...niseme kwamba, wivu unazidi!
“Unajua unapokuwa msanii,
unakuwa na mambo mengi, shoo kibao kila week-end, safari za mikoani nazo
hazina idadi, club ndio usiseme, sasa kwa hali hiyo, lazima uwe na
mwanamke smart kwa kila kitu.
“Tuongee ukweli, hakuna mtu anayekubali
kuwa na mpenzi tapeli, sisi hatuna matatizo, lakini kama umefuata jina
langu au pesa, nitakushtukia soon na hapo ndipo nitakapompiga kibuti na
maisha yanaendelea,” ndivyo mmoja wa kinara katika Bongo Fleva
anavyosema.
Hebu sikia kauli ya msanii huyu wa filamu: “Wanawake
wanapenda umaarufu wetu, kwahiyo ukiwa naye siku mbili, ukimshtukia
unamtema, hapo ndipo penye tatizo bro. Mimi sihitaji mtu anayependa jina
langu, nahitaji penzi la dhati.”
TATIZO NI NINI?
Kikubwa
ni katika KUELEWA na kutofautisha mapenzi na ustaa. Kama umempenda,
umpende kwa mapenzi ya dhati, achana na ustaa wake, lakini lazima umjue
mwenzi wako na uende naye jinsi anavyotaka.
Mapenzi ya kitapeli au
kufuata mali na umaarufu hayana nafasi kabisa katika maisha ya sasa,
yote yanawezekana lakini kwa kukubali kujifunza na kubadilika kulingana
na mwenzi wako alivyo.
UPO KWENYE UHUSIANO NA STAA?
Kama
nilivyotangulia kusema awali, sina maana kwamba mastaa wote hawawezi
kuishi na wenzi wao bila kuwepo kwa migogoro, ni baadhi yao! Pamoja na
kuwa na migogoro hiyo ambayo mwisho wake mara nyingi imekuwa ni
kuachana, hakumaanishi kwamba, mastaa hawafai kuwa na wapenzi.
Hapa
nataka kuzungumza na wale ambao tayari wapo katika uhusiano na mastaa na
wale ambao wanatarajia kuwa na wenzi wenye majina makubwa kwenye jamii.
Hebu pitia vipengele vifuatavyo;
Usiwe na wivu sana!
Ni
kweli kwamba, kati ya alama za mapenzi ya dhati ni pamoja na wivu,
lakini unapokuwa na uhusiano na mwenzi staa, lazima upunguze wivu. Hii
haina maana kwamba, umuache awe kicheche, awe na mapatna wengi, hapana!
Mara
nyingi mastaa huwa wanaiga mambo ya Kizungu, mathalani husalimiana kwa
kukumbatiana, kuandikiana sms kwa maneno ya mapenzi kama dear, sweetie,
mpenzi n.k, ukikutana na mazingira kama hayo, kuwa mpole, lakini fanya
uchunguzi wako taratibu bila ya yeye kujua. Penye ukweli, uongo
hujitenga.
0 comments :
Post a Comment