Msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni Sylivery aka Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA ambaye amefariki siku ya juzi February 28.
Leo Mpoki amesikika akizungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu
akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu
unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda
Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu
yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu”
“Imeniathiri
kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini
ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga
mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa
wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..“
“mwisho
wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna la kufanya kuhusu
yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi lisimvunjie
heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na watu
wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..“
0 comments :
Post a Comment